×

Kivumbi leo Mkwakwani Fainali ya Ngao ya Jamii kati ya Yanga na Simba

KUELEKEA mchezo wa fainali ya Ngao ya Jamii kati ya Yanga na Simba unaotarajiwa kuchezwa leo Jumapili kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, makocha wa timu hizo wamejikuta wakitambana, huku kila mmoja akisema ataipa ushindi timu yake.

Simba leo Jumapili, wataingia katika mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza michezo miwili mfululizo ya Ngao ya Jamii mbele ya Yanga.

Akizungumza na Spoti Xtra, Kocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ alisema: “Ni furaha kubwa kwetu kufika katika hatua ya fainali, kikubwa ambacho tunahitaji ni kupata matokeo mazuri, tunafahamu hii ni dabi ambayo huwa na ugumu wake, lakini tayari tumeiandaa timu kwa ajili ya kupata ushindi.

“Tunawaheshimu wapinzani wetu kwa kwani wamekuwa na kiwango bora katika mchezo uliopita, Simba sisi tunatambua kuwa ni kwa kiasi gani mashabiki wetu wanahitaji tupate matokeo mazuri, na sisi tunawaahidi hilo na tuna nia kubwa.”

Kwa upande wa Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi, alisema: “Nafurahia kucheza na Simba, nafurahia kucheza kwenye hii dabi, hivyo niwaambie tu mashabiki ambao pengine wanasema kuwa hofu ni kubwa, wanatakiwa kufahamu kuwa nimecheza dabi kubwa Afrika, hivyo wala sina presha na badala yake naiandaa timu yangu kwenda kupata matokeo ya ushundi.”

STORI NA MARCO MZUMBE, TANGA

Leave a Comment