Msanii wa mkongwe wa Bongo Muvi ambaye amecheza filamu nyingi,Eva Clement @da_pendoo amefunguka ukweli kuhusiana na kifo cha aliyekuwa mfanyakazi wake katika kampuni ya kuuza vifaa vya mahospital na mashule, Alex Korosso ambaye alijiua kwa kujipiga risasi miaka miwili iliyopita,baada ya kumpiga risasi kijana aliyekuwa akimuamulia ugomvi, kwenye baa moja iliyokuwepo Sinza Mori, kuzua maswali mengi sana ya nini kilimsibu.
Msanii huyo na mfanyabiashara pia aliweka wazi alipofanyiwa mahojiano na @globaltvonline kupitia mtangazaji wake @imeldamtema kuwa Alex,hakuwa na deni lolote wala kuwa na shida yoyote ya kifedha na wala hakuwa ugomvi na mwanamke au chochote kinachohusiana na mapenzi.