×

Kamati Ya Amani Dar, Yawaasa Watanzania Kutoshawishiwa Kuvuruga Amani

Mwenyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa wa Dar es Salaam, Shekh Walid Alhad Kawambwa ambaye ni Shekh Mkuu wa Mkoa wa Dar, akizungumza kwenye mkutano huo mapema leo.

Dar es Salaam, 17 Agosti 2023: Kamati ya Amani mkoa wa Dar es Salaam inayoongozwa viongozi wa dini ya kiislamu na kikristu chini ya Mwenyekiti wake, Shekh Walid Alhad Kawambwa ambaye ni Shekh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, leo imewaasa Watanzania kutoshiriki vurugu zinazochochewa na baadhi ya watu kwa kupitia mgongo wa kisiasa na mengineyo.

Shekh Walid amesema kwaniaba ya kamati hiyo wameamua kuwaasa Watanzania kutoshawishika na maneno ya wanaohamsisha vurugu kwa masirahi yao binafsi.

Mkutano huo ukiendelea.

Shekh huyo amesema hayo kufuatia taarifa ya hivi karibuni iliyotolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Cammilius Wambura juu ya watu hao wanaotaka kuvuruga amani ya hapa nchini.

Shekh Walid amesema hivi karibuni wameibuka watu wanaotumia njia mbalimbali ikiwemo mikutano ya kisiasa na kutaka kuhamasisha vurugu kwa kufanya maandamano ya nchi nzima.

Shekh huyo amewaasa vijana na watu wa rika mbalimbali wasikubali kutumika katika kuharibu amani ya nchi ambayo tumedumu nayo kwa miaka mingi na kuifanya nchi yetu kuwa kimbilio la nchi zisizo na amani na utulivu.

“Nchi inapoingia kwenye machafuko hakuna atakayesalimika kama si wewe basi ndugu na jamaa zako ni lazima wadhulike na machafuko hayo.

“Hivyo tusiwachekee hao wanaotaka kutuvurugia amani ya nchi yetu, tunachotakiwa ni kulinda amani na utulivu tulionao na kumuunga mkono, Rais wetu, Dkt Samia Suluhu Hassan katika ujenzi wa taifa letu”.

Katika mkutano huo na wanahabari upande wa Wakristu uliwakilishwa na Askofu Bendela na wakristu wengine kutoka katika madhehebu tofauti.  HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS NA ISSA MNALLY 

Leave a Comment