
SENETA wa Uasin Gishu, Jackson Mandago, na Watu wengine 3 wanakabiliwa na Mashtaka 11, ikiwa ni pamoja na Wizi na matumizi mabaya ya Ofisi
Anatuhumiwa kushiriki katika njama ya kuiba Ksh. Bilioni 1.1 (Tsh. Bilioni 19.13) kwenye Akaunti ya Benki ya Biashara ya Kenya tawi la Eldoret ambazo zilikusudiwa kugharamia Elimu ya Vyuo Vikuu kwa Wanafunzi wa Kenya kwenda kusoma Nchini Finland na Canada wakati akiwa Gavana
Ubadhirifu huo ulisababisha Mamia ya Wanafunzi kukwama Nchini Kenya, huku wale ambao walikuwa wameshaanza Masomo yao nje ya Nchi kuwa hatarini kukosa Makazi, Kufukuzwa, na Kurejeshwa Nyumbani baada ya Serikali ya Kaunti ya Uasin Gishu kusitisha Malipo ya gharama za Masomo na Malazi
Aidha, Rais William Ruto ameagiza yeyote anayehusika na Ubadhirifu kulipa haraka Fedha hizo au atakabiliwa na matatizo, huku akiahidi Ufadhili wa Masomo katika Vyuo vya Ndani kwa Waathirika mara baada ya Uchunguzi wa suala hilo kukamilika.