
Askofu wa Dayosisi ya Karagwe ya kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dk. Benson Bagonza amempongeza Rais Samia kwa uongozi wake shupavu Tangu aingie madarakani na hasa kwa kuwa na moyo wa ustahimilivu na wenye busara katika maamuzi yake.
Ameyasema hayo leo Agosti 21, 2023 jijini Arusha ambapo yeye na viongozi wengine wa kidini wa kanisani la kilutheri wanatagemea kufanya maadhimisho ya miaka 60 ya kanisa la KKKT katika viwanja vya chuo kikuu cha Tumaini Na mgeni Rasmi akiwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
View this post on Instagram