×

Askofu Shoo: Kuhusu Dp World, KKKT Inaunga Mkono Uwekezaji – Video

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo kutoka Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Askofu Fredrick Shoo ikiwa ni kwa ajili ya jitihada zake za kuleta Maendeleo nchini wakati wa Maadhimisho ya miaka 60 ya Kanisa hilo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Viwanja vya Mfuko wa Wastaafu Mkoani Arusha tarehe 21 Agosti, 2023

Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dkt. Fredrick Shoo amesema “Ileweke wazi kwamba Kanisa linaunga mkono uwekezaji unaofanywa Nchini licha ya kutambua kuna maoni mbalimbali kutoka kwa Wadau tofauti.”
Kuhusu uwekezaji wa DP World ameongeza “Viongozi wa Dini zote kwa uwakilishi tuliomba kuja kukuona (Rais Samia) mwanzoni mwa jambo hili, kwa ungwana ukatupokea na tukakukabidhi maoni yetu na ukaahidi utayawasilisha kwa wataalam kufanyiwa kazi kwa maslahi mapana ya Taifa.”
Amesema hayo mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan katika Maadhimisho ya Miaka 60 ya KKKT katika Chuo cha Tumaini Makumira Mkoani #Arusha, leo Agosti 21, 2023

Leave a Comment