
WINGA wa Simba, Aubin Kramo amezua gumzo kubwa mara baada ya kushindwa kucheza ndani ya kikosi hicho tangu asajiliwe katika michezo ya karibuni.
Kramo mara ya mwisho kucheza ilikuwa ni katika mchezo wa Simba Day ambapo aliingia katika dakika za mwisho wakati Simba ikiumana na Power Dynamo kutoka Zambia na kushinda mabao 2-0.
Licha ya mchezaji huyo kushindwa kucheza jambo ambalo liliwafanya mashabiki wa Simba kuhoji kwa muda wakitaka kufahamu kwa nini mchezaji huyo hachezi ingawa alipotoka katika klabu ya Asec Mimosas amefanya makubwa.
Championi Jumatatu lilimtafuta daktari wa Simba, Edwini Kagabo ambaye ameelezea hali ya kikosi cha Simba na kumtaja winga huyo kuwa ni majeruhi hivyo ambapo alipata changamoto katika mchezo wao dhidi ya Singida Fountain Gate kule Tanga huku akiweka wazi kuwa wanampa muda kwa ajili ya maandalizi ya michezo mingine.
“Kramo alipatwa na changamoto binafsi akiwa anajiandaa na mchezo wetu dhidi ya Singida kule Tanga mchezo wa Ngao ya Jamii, hivyo kwa upande wetu sisi na jopo zima la madaktari tumeona tumpe muda mzuri wa kujiandaa tayari kwa michezo mingine.
“Kikubwa yupo katika hali nzuri ya uangalizi kwahiyo ni jambo la jopo la madaktari na kama atakuwa sawa basi muda wowote atamuona akipata nafasi ya kucheza,” alisema daktari huyo.
STORI NA MARCO MZUMBE,