×

Greenwood Ndio Basi Tena, Anaondoka United

HATIMAYE fowadi wa Manchester United, Mason Greenwood ataondoka katika klabu hiyo kwa makubaliano ya pande zote mbili baada ya uchunguzi wa ndani wa miezi sita kuhusu mwenendo wake kukamilika.

Greenwood alikamatwa Januari 2022 kufuatia madai yanayohusu unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya mpenzi wake ikiwa ni pamoja na kujaribu kubaka na kushambulia lakini yalitupiliwa mbali Februari 2, mwaka huu.

United ilisema katika taarifa yake: “Wale wote wanaohusika, ikiwa ni pamoja na Mason, wanatambua ugumu wa yeye kurejesha maisha yake ya Manchester United.

“Kwa hivyo imekubaliwa kuwa itakuwa sahihi zaidi kwake kufanya hivyo nje ya Old Trafford, na sasa tutashirikiana na Mason kufikia matokeo hayo.

“Kulingana na ushahidi tulionao, tumehitimisha kuwa shutma zilizochapishwa mtandaoni hazikutoa picha kamili na kwamba Mason hakufanya makosa ambayo alishtakiwa hapo awali.”

Katika taarifa yake, Greenwood alikubali kwamba alifanya makosa na akaongeza: “Sikufanya mambo niliyoshutumiwa.”

Aliongeza: “Uamuzi wa leo umekuwa sehemu ya mchakato wa ushirikiano kati ya Manchester United, familia yangu na mimi. Uamuzi bora kwetu sote ni mimi kuendelea na maisha yangu ya soka nje ya Old Trafford.”

Tetesi zilizopo kwa sasa inadaiwa staa huyo anatakiwa na Al-Ettifaq ya Saudi Arabia kwa pauni milioni 10 huku Roma inayonolewa na Jose Mourinho nayo ikihusishwa.

JWTZ WATANGAZA KIAMA – ”SALIMISHENI SARE za JESHI NDANI ya SIKU 7 KWENYE VITUO VYA POLISI”…

Leave a Comment