×

Fei Toto Atajwa Azam Kutolewa Kombe la Shirikisho Afrika Hatua ya Awali

Feisal Salum ‘Fei Toto’.

BAADA ya Azam FC kuondolewa katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya awali, kocha wa timu hiyo, Yousouf Dabo, amesema sababu kubwa iliyofanya kutokea hali hiyo ni matumizi mabaya ya nafasi walizopata wachezaji wake.

Juzi Ijumaa, Azam iliondolewa na Bahir Dar Kenema ya Ethiopia kwa penalti 4-3 baada ya matokeo ya jumla kuwa 3-3. Mchezo wa kwanza ugenini Azam walifungwa 2-1, nyumbani wakashinda 2-1.

Feisal Salum ‘Fei Toto’, Prince Dube na Idd Nado, waliongoza safu ya ushambuliaji ya Azam katika mchezo wa juzi ambao licha ya dakika tisini kushinda 2-1, lakini wakakwama kwenye penalti, huku wakikosa nafasi nyingi za kufunga.

Akizungumza na Spoti Xtra, Dabo alisema: “Ukitazama michezo yote miwili utagundua tulipata nafasi nyingi, lakini wachezaji hakuwa makini katika kuzitumia, kama tungezitumia vizuri basi tungesonga mbele, naamini kama tungebadili zile nafasi kuwa mabao basi tungekuwa tunaongea mambo mengine.”

Leave a Comment