×

Washindi Wa Kampeni ya Tigo Chawote Wapewa Chao

Ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya chawote ya Tigo  imekabidhi washindi sita hundi ya milioni moja moja  ofisini kwao Jijini Dar es salaam.

Zaidi ya washindi elfu ishirini mia moja na sitini  na kila siku washindi mia tatu ishirini wanashinda milioni moja. Hayo  wameyasema mabalozi wa Promosheni hiyo, Millard Ayo na Hamisa Mobeto.

Mshindi wa   Milioni moja  mkazi Lucas Mtei wa Dar es Salaam amesema  fedha hizo zitamsaidia kuongeza mtaji wake wa biashara  kwani yeye ni mjasiriamali.

Mabalozi wa promosheni hiyo, Hamisa Mobeto na Millard Ayo wakiwa na mmoja ya washindi.

Naye Angel Samwel mshindi wa milioni moja ameongezea kwa kusema  fedha hizo zitamsaidia kuongeza kwenye mtaji wa biashara yake.

Sanjari na hayo washindi wengine ambao ni Maua Ally, Raymond January, Milka Sanga, Mwajabu Mbwana wamesema fedha hizo zitawasaidi kwenye biashara zao na mambo binafsi.

Promosheni hiyo ya chawote itadumu kwa siku tisini hii ikiwa  ni wiki ya tisa mshindi wa mwisho wa mwezi anashinda milioni tano mbali na zawadi za fedha taslim wanazotoa nyingine ni bonus,dakika na sms zikiwa zimesalia wiki nne promotioni hiyo kuweza kuisha.

Leave a Comment