
Mkurugenzi Mkuu mpya wa Idara ya Usalama wa Taifa Balozi Ali Idd Siwa amekuwa katika utumishi wa umma tangu mwaka 1977 na kati ya mwaka 2001-2014 Ndugu Siwa alikuwa Afisa Mambo ya Nje Mkuu katika ofisi ya Ubalozi wa Tanzania Abu Dhabi iliyoko Umoja wa Falme za Kiarabu (United Arab Emirates); Moscow, nchini Urusi na baadaye Berlin, nchini Ujerumani.

Ndugu Ali Idd Siwa Agosti, 2014 Rais Jakaya Kikwete alimteua kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kigali, nchini Rwanda akichukua nafasi ya Balozi Dkt Mwita Marwa Matiko. Majukumu aliyoendelea nayo pia mwaka 2018-2021 baada ya kuteuliwa na Rais John Pombe Joseph Magufuli kabla ya kurejea nchini na kuteuliwa kuiongoza bodi ya Mfuko wa NSSF na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Katika nafasi mbalimbali alizotumikia ametajwa kuwa mtu mahiri katika utendaji kazi wenye uadilifu, uzalendo, ubunifu na matokeo makubwa.
https://globalpublishers.co.tz/uteuzi-balozi-ali-idi-siwa-mkurugenzi-mpya-wa-idara-ya-usalama-wa-taifa/