
Droo ya kupanga makundi ya michuano ya Klabu Bingwa Ulaya kwa msimu wa 2023/24 imechezeshwa leo ambapo Bingwa Mtetezi, Man. City amepangwa Kundi G linaloonekana kuwa jepesi kwake
Manchester United imeangukia Kundi A pamoja na Vigogo wa Ujerumani, Bayern Munich. Newcastle inayorejea kwenye michuano hiyo kwa mara ya kwanza tangu ishiriki msimu wa 2002/03 imepangwa kundi la kifo
