×

Ali Bongo yuko Huru na Anaweza Kuondoka Gabon, Atangaza Jenerali Oligui

Rais wa Gabon aliyeondolewa madarakani, Ali Bongo Ondimba

Rais wa Gabon aliyeondolewa madarakani, Ali Bongo Ondimba, yuko huru kufanya anachokitaka na anaweza kwenda nje ya nchi, ikiwa anataka, Kanali Ulrich Manfoumbi Manfoumbi ametangaza kwenye televisheni ya serikali, akisoma taarifa kwa vyombo vya habari iliyotiwa saini na Jenerali Oligui, ambaye sasa anaongoza taifa hilo.

Ali Bongo, madarakani kwa miaka 14, alikuwa chini ya kizuizi cha nyumbani tangu mapinduzi ya kijeshi ya Agosti 30, yaliyotekelezwa bila umwagaji damu chini ya saa moja baada ya kambi yake kutangaza kuchaguliwa kwake tena katika kura iliyoelezwa kuwa ya udanganyifu na viongozi wa mapinduzi.

“Kwa kuzingatia hali yake ya afya, aliyekuwa Rais wa Jamhuri Ali Bongo Ondimba yuko huru kufanya anachotaka. Anaweza, akipenda, kwenda nje ya nchi kufanya uchunguzi wake wa afya,” taarifa hiyo kwa vyombo vya habari imeongeza.

Ali Bongo alipatwa na kiharusi kibaya mnamo mwezi Oktoba 2018 ambacho kilimfanya adhoofike kimwili, huku mguu wake wa kulia na mkono hasa akivitumia kwa shida.

BALAA TUPU MSAFARA wa NAIBU WAZIRI MKUU BITEKO -ATINGA OFISINI, AWACHANA MAKAVU WANAOJIFANYA MANABII


 

Leave a Comment