
Zaidi ya washindi elfu ishirini na sita wameshinda kwenye kampeni ya Tigo ya Chawote hayo ameyasema Mary Rutta Meneja wa wateja maalum Tigo pesa Septemba 15, 2023 wakati akikabidhi hundi ya milioni moja kwa washindi hao kwenye Ofisi za Tigo Jijini Dar es Salaam.

Marry Kavishe mshindi wa milioni moja ya kampeni hiyo ya chawote amesema fedha hizo zitamsaidia kununua mashine ya cherehani na kukuza biashara yake.
Naye Kenedy Shao amesema baada ya kupokea mkwanja alisema fedha hizo zinasaidia kumlipia mtoto ada ya shule na zitakazobaki ataangalia mambo mengine.

Kwa upande wao Adam Peter na Abasi Mwinyi wamesema fedha hizo zitawasaidia kukuza biashara zao na mambo mengine muhimu.

Kampeni hiyo inadumu kwa takribani siku tisini mbali na fedha taslim wanazotoa zawadi nyingine ni Bonus, Dakika nk.