
Mabingwa watetezi wa kombe la Shirikisho Afrika, USM Alger wametwaa kombe la CAF Super Cup 2023 kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Al Ahly katika dimba King Fahd, Riyadh Saudi Arabia.
FT: Al Ahly 🇪🇬 0-1 🇩🇿 USM Alger
⚽ Zineddine Belaid (P) 42′
USM Alger wametwaa kombe CAF Super Cup kwa mara ya kwanza kihistoria ikiwa ni kombe lao la pili kwenye michuano ya Afrika.