
Nachukua fursa hii kumshukuru Mungu kwa kuweza kutupa afya na kuweza kumujuika hapa siku ya leo kwenye uzinduzi wa wiki ya wateja kwa mwaka 2023. Nawashukuru sana Wateja wetu ambao wamekuwa na waaminifu siku zote kwa kuendelea kutumia huduma zetu mbali mbali za Airtel. Kwa hakika nyinyi ni watu muhimu sana kwenye maendeleo yetu na sisi Airtel Tanzania tutaendelea kuwahudumia na bidii pamoja na kuhakikisha mnapa huduma iliyo bora kabisa.
Kwa njia ya kipekee naomba nimpongeze Mgeni wetu, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Hashimu Komba kwa kuweza kutenga muda wako na kuja kujumuika nasi hapa kwenye ufunguzi wa maadhimisho ya wiki ya wateja licha ya kuwa na shughuli nyingi kama kiongozi na mkuu wa wilaya huu mkubwa wa kibiashara wa Dar es Salaam. Asante sana na karibu Mhe mgeni rasmi.
Sisi Airtel siku zote tumekuwa tukichukua na kutambua mteja kama nguzo ya ukuaji wa biashara yetu kama watoa huduma za mawasiliano hapa nchini Tanzania. Kwa sababu hiyo, huduma na bidhaa zetu zimekuwa ni suluhisho la huduma za mawasiliano.

Tunafanya kazi bega kwa bega na Serikali ili kuweza kufanisha malengo yetu kwa pamoja. Serikali imekuwa msitari wa mbele kuhakikisha kuwa Watanzania wanaenda samba samba na ulimwengu wa kidigitali kwa kuwawezesha kuwa na simu janja na kwa sababu hiyo ikaamua kufuta tozo kwenye simu njanja. Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kutambua hilo imekuja na mpango kambambe ambapo Mtanzania hata hana pesa ya kutosha ya kuweza kununua simu njanja, anaweza kuipata kwa kulipa kiasi na kinachobakia anamalizia kidogo kidogo. Simu zetu njanja za mkopo zinapatikana kwa kulipia kiasi cha elfu 70, kasha mteja ana uwezo wa kumiliki kwa kulipia kiasi cha elfu moja kila siku au elfu saba kila siku. Simu hizi zinakuja na ofa kabambe za intaneti pamoja na muda wa maongezi.
Na hili kuendelea kutoa huduma kwa haraka pamoja na kuleta huduma zetu karibu na wateja, kampuni ya Airtel imeweza kufungua maduka ya Airtel Zaidi ya 42,000 kote nchini pamoja na Airtel Money branches 3,500, Mawakala Zaidi ya 200,000. Hii ni kuhakikisha kuwa Mtanzania yeyote atapata huduma zetu mahali popote pale alipo.
Napenda kuwafahamisha ya kuwa kwa sasa ukiwa na Airtel Money unaweza kutuma na kupokea fedha kutoka na kwenda kwenye nchi zaidi ya 200 duniani moja moja kupitia akaunti yako ya Airtel Money. Hii inamaanisha ya kwamba hakuna sababu tena ya kuendelea kuhatarisha maisha yako kwa kutembea na kiasi kikubwa cha fedha mkononi.

Kama ilivyo kauli mbiu ya wiki ya huduma kwa wateja ya mwaka ‘Team Service’, Airtel tunafanya kazi kwa pamoja kama familia ili kuhakikisha ya kwamba huduma na bidhaa mbali mbali kutoka kwetu zinaendelea kuwa za kiwango kikubwa zaidi.
Ndugu Mgeni rasmi, naomba nikufahamishe ya kwamba kampuni ya Airtel Tanzania inamilikiwa na Watanzania kwa asilimia 49 kupitia kwa Serikali yao. Ni furaha kwa hivyo kutambua ya kwamba wakati wowote pale mnapokuwa mnatumia huduma za Airtel basi mtambue ya kwamba mnatumia kilicho cha kwenu.
Naomba nikimalizia nitoe rahi kwa Watanzania pamoja na wateja wakati tukiendelea kusherehekea wiki ya huduma kwa wateja kuwa sisi Airtel tutawasiliana na mteja kwa kupiga simu kupitia namba ya yetu ya huduma kwa wateja ambayo ni +255 100 na sio vinginevyo. Pia wakati wa promosheni zetu ushiriki huwa ni bure na hakuna gharama yoyote ya kulipia ili kupata zawadi yako kwani kwa washindi sisi Airtel tunakuletea pale ulipo. Usitoe taarifa zozote kuhusu akaunti yako ya Airtel Money au kumpa mtu namba yako ya siri ya akaunti ya Airtel Money.
Asanteni sana kwa kunisikiliza na kwa nafasi ya kipekee naomba nimkaribishe Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Hashimu Komba aweze kutufungulia wiki ya huduma kwa wateja pamoja na kuongea na sisi.

Kwa uapnde wake Mkuu wa Wilaya ya Ungu alisema kuwa:
Ndugu Watanzania, nina uhakika mmesikia ya kuwa kampuni ya Airtel inamilikiwa na sisi Watanzania kwa asilimia 49. Ni furaha kutambua ya kwamba kumbe hata sisi Watanzania tunao uwezo wa kumiliki kampuni yenye mafanikio makubwa kama Airtel. Sasa niwaombe chonde chonde tuendelee kutumia huduma za Airtel kwa wingi kwani kwa kufanya tunazidi kuchangia pato la taifa kwani kila wakipata Airtel na sisi tunapata.
Nimefurahi kusikia ya kwamba Airtel mnao maduka zaidi ya 4,500 nchini kote pamoja na Airtel Money branches 3,200, mawakala zaidi 200,000. Hii inaonyesha ni kiasi ngani mmefanya kazi kubwa ya kuwekeza kwenye kupanua mtandao wenu. Nimepata taarifa zaidi ya kuwa kwa sasa kuna huduma nyingi ambazo zamani mteja alikuwa analazimika kwenda kwenye ofisini zeni kupata. Kwa mfano kurundisha muamala uliotumwa kimakosa au kupata token za LUKU kwa sasa mteja anaweza kujihudumia. Hongereni sana kwa hilo.
Huduma za simu mkononi kwa sasa sio anasa tena. Sisi zote kila mtu kwa nafasi yake anahitahi mawasiliano. Kwa wafanya biashara kuweza kuongeza kipato chao kwani wanapata hali ya bidhaa sokoni kupitia simu zao mpaka kwa wanafunzi. Hii pia inaendana na ukuaji wa uchumi wa kidigitali. Watanzania na hasa wakazi wa mkoa wa Dar es Salaam naomba tuendelee kuwa mbele kwenye matumizi ya kidigitali bila kubaki nyuma na hivyo ndio ulimwengu unavyotaka.
Nimeweza kutembelea na kujionea maonyesho yenu hapa Airtel. Kwa hakika yamefana sana na nimefuhia mno.
Naomba nitumia nafasi hii kusema kuwa sherehe za wiki ya huduma kwa kampuni ya Airtel zimefunguliwa rasmi na nitoe rai kwa wakazi wa Dar es Salaam kuja kutembelea kwenye viwanjwa hizi za Mbagala na kuweza kujionea huduma na bidhaa mbali mbali za Airtel.