
Dar es Salaam, 4 Oktoba 2023: Ikiwa ni mwendelezo wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma Kwa Wateja, leo viongozi wa Kampuni ya Tigo Tanzania akiwemo Mkurugenzi Mtendaji Bwn. Kamal Okba wamewatembelea kitengo cha huduma kwa wateja na kuwapongeza kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuwahudumia na kuwasikiliza wateja wa Tigo masaa 24 kupitia namba 100, aidha viongozi hao wamesikiliza changamoto mbalimbali zinazowasilishwa na wateja kupitia watoa huduma hawa na kuahidi kuzifanyia kazi.

Sambamba na hilo viongozi hao wamewatembelea na kuwahudumia wateja wa Tigo waliokuwepo katika duka la Tigo Palm Village, tukio liliambatana na ukataji wa keki kama ishara mojawapo ya kuwashukuru kwa kuchagua kutumia mtandao huo ulishika namba kwa kutoa huduma mwaka huu.
Akizungumza baada ya viongozi hao kuyatembelea maeneo hayo muhimu, Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma Kwa Wateja Tigo, Bi. Mwangaza Matotola amesema;

“Leo tumeunganika na viongozi wetu kwa ajili ya kuwashukuru wateja na watoa huduma wetu kwa kuendelea kutuamini na kututhamini, tuliianzia wiki hii ya huduma kwa wateja tukiwa mkoani Iringa na tumekua tukienda sehemu mbalimbali kuwashukuru watoa huduma na wateja wetu, kwetu sisi mteja ni nguzo kubwa ya kampuni. Napenda kutumia nafasi hii kuwatakia heri ya wiki ya huduma kwa wateja”. Alimaliza kusema.

Naye mmoja wa wateja wa Tigo aliyekutwa na msafara wa viongozi wa Tigo kwenye duka hilo la Palm Village ambaye alijitambulisha kwa wadhifa na jina la CPA Optatus Luoga akizungumza na wanahabari ameipongeza kampuni ya Tigo kwa huduma zao.

CPA Luoga ambaye ni mmiliki wa shule ya Locee Pre & Primary ambayo imeshika nafasi ya pili mwaka jana katika matokeo ya darasa la saba na kushika nafasi ya kwanza kwa darasa la nne mwaka jana amesema anatumia huduma za Tigo kwa miaka mingi kutokana na huduma zao nzuri ikiwemo intaneti yenye kasi, huduma ya kutuma ujumbe wa pamoja unaomraisishia kuwatumia ujumbe wa pamoja wateja wake na kupatika kiuhakika nchi nzima.