×

SGA Yapokea Tuzo Ya Juu Kwa Kuwekeza Katika Teknolojia

Makamu wa Rais wa Pili wa Zanzibar, Mh. Hemed Suleiman akiwapungia wafanyakazi wa SGA Security wakati akipita karibu na banda la kampuni hiyo katika maonesho ya Kimataifa ya Madini yaliyomalizika hivi karibuni Mjini Geita. Kampuni ya SGA Security imepokea tuzo kwa utoaji wa huduma bora za ulinzi unaotumia teknolojia ya kisasa migodini.

Tuzo hiyo ilitolewa kwa SGA wakati wa maonesho ya Kimataifa ya Madini yaliyomalizika Mjini Geita hivi karibuni.

Maonesho hayo ya sita, yaliyodumu kwa siku 10, yalifungwa na Makamu wa Rais wa pili wa Zanzibar Mh. Hemed Suleiman na yalikusanya washiriki zaidi ya 350.

Washiriki hao walipata fursa ya kushuhudia jinsi gani teknolojia na binadamu vinaweza kutumika kwa moja katika masuala ya ulinzi wa mali migodini.

Mkurugenzi Mtendaji wa SGA Security, Eric Sambu, aliwapongeza waandaaji wa maonesho hayo kwa maandalizi mazuri na kwa kutambua mchango wa SGA Security.

 “Tuzo hii inadhihirisha juhudi zetu katika kuhakikisha ulinzi na usalama wa kutosha katika maeneo ya migodi ili wahusika wakuu katika eneo hilo wajikite vikamilifu katika biashara,” alisema.

Makamu wa Rais wa Pili wa Zanzibar, Mh. Hemed Suleiman akiwapungia wafanyakazi wa SGA Security wakati akipita karibu na banda la kampuni hiyo katika maonesho ya Kimataifa ya Madini yaliyomalizika hivi karibuni Mjini Geita.

Alisema kampuni hiyo imewekeza sana katika ubia na makampuni makubwa yanayotengeneza vifaa vya ulinzi wa kielektronia ili kuhakikisha wateja wa SGA wanapata huduma bora kwa bei nafuu. “Siri yetu kuu ni mafunzo tunayotoa kwa mafundi wetu ili waendelee kuwapa wateja huduma bora inayoendana na fedha walizowekeza katika teknolojia hizi,” alisema.

Mkurugenzi Mtendaji wa SGA Tanzania, Eric Sambu (katikati) na baadhi ya wafanyakazi wa SGA Security wakionesha tuzo iliyokabidhiwa kwa kampuni hiyo katika maonesho ya Kimataifa ya Madini yaliyomalizika Mjini Geita hivi karibuni.

SGA ilitambuliwa na Wizara ya Madini mwaka jana pia katika Warsha ya Madini kwa kuthamini vitu vya ndani ya Tanzania. “Tunajivunia katika kuajiri wazawa na hata bidhaa tunazotumia katika shughuli zetu ni za ndani pia,” aliongeza Bw. Sambu.

SGA Security ilikuwa kampuni ya kwanza kuazisha utoaji wa huduma binafsi za ulinzi nchini Tanzania miaka 40 iliyopita. Kwa sasa imeajiri wafanyakazi wa kitanzania wapatao 5000 katika matawi yake yote nchini.

Kampuni hiyo inatoa ulinzi wa hali ya juu na wa uhakika katika kusafirisha vitu vya thamani, ulinzi, alarm na uwekaji wa vifaa vya ulinzi wa kielektroniki.

SGA pia ina cheti cha hadhi ya ISO na imeendelea kujishindia tuzo mbalimbali ndani na nje ya nchi kutokana na huduma zake zenye ubora.

Leave a Comment