×

Mwakinyo Afungiwa Mwaka Mmoja na Kamisheni ya ngumi Nchini

Kamisheni ya ngumi za kulipwa Nchini (TPBRC) kupitia Kamati yake ya Nidhamu imetangaza kumfungia Bondia Hassan Mwakinyo kwa kipindi cha mwaka mmoja kwa kosa la kushindwa kupanda ulingoni kwenye pambano lililoandaliwa na kampuni ya uandaaji wa michezo ya PAF.

Akitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari Katibu Mkuu wa TPBRC, George Lukindo amesema, mbali na adhabu hiyo Mwakinyo ameamriwa kulipa faini ya Shillingi Milioni 1 na adhabu hiyo inaanza leo Oktoba 10 mwaka 2023 na kumalizika Oktoba 10 mwaka 2024.

Mwakinyo amepewa nafasi ya kukata rufaa ndani ya kipindi cha siku 7 kuanzia siku ya kutangazwa hukumu hiyo.

HATARI! NAGWA ANUSURIKA KUCHOMWA MOTO, KISA WIZI? MKOJANI AMJIA JUU KISA UMBAMBAMBA….

Leave a Comment