×

Mfanyabiashara Maarufu Arusha Akutwa Amefariki Kwenye Gari – Akutwa Na Maburungutu Ya Pesa -Video

Mfanyabiashara maarufu wa maduka ya simu Jijini Arusha aliyefahamika kwa jila moja la Mzee Malya amekutwa amefariki kwenye gari yake katika eneo la maegesho ya magari (City Car Wash) huku mwili wake ukiwa umeharibika.

Tukio la kugundulika kwa mwili wa marehemu limetokea mapema leo baada ya waosha magari kusikia harufu kali iliyokuwa ikitoka ndani ya gari hilo Askari Polisi walifika eneo la tukio na kuukuta mwili huo uliokuwa kwenye gari aina ya SCUDO lenye namba T 466 AUB lililokuwa limeegeshwa katika eneo hilo.

Baadhi ya Mashuhuda wamedai marehemu Malya amekuwa na desturi ya kufika eneo hilo na kuegesha gari lake na kisha kwenda bar iliyopo eneo hilo kwa ajali ya kula chakula na kunywa.

Mwenyekiti wa eneo hilo maarufu kwa wauzaji wa magari (Madalali) Alex Kahela alisema alipata taarifa asubuhi ya Oktoba 13, kuhusiana na tukio hilo na baada ya kufika aliweza kulitambua gari hilo kuwa ni mali ya Mfanyabiashara huyo.


CHOTA MAPENE ndiyo mchongo mpya town! Kwa shilingi 1,000 tu, yaani BUKU unajichotea mapene kibao au kupata nafasi ya kujishindia ZAWADI MBALIMBALI KILA SIKU, KILA WIKI kupitia Global TV, Global Radio na mitandao ya kijamii! ======================== Ingia kwenye simu yako📲, sehemu ya kufanyia malipo, andika namba ya kampuni 553111, kumbukumbu namba 255 au andika neno GLOBAL. Weka kiasi cha shilingi 1,000, weka namba yako ya siri, thibitisha na tuma.👍 PEASA UTATUMIWA MOJA KWA MOJA KWENYE SIMU YAKO!🤝👍💰

Leave a Comment