×

Rais Samia Azindua Rasmi kituo cha Polisi wilaya ya Ikungi mkoani Singida – Video

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni, Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP) Camillus Wambura pamoja na viongozi wengine wakati akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Jengo la Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida tarehe 15 Oktoba, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amezindua rasmi kituo cha Polisi wilaya ya Ikungi mkoani Singida.

Ambapo Rais Dkt. Samia aliwataka askari Polisi kutumia kituo hicho kwa kutoa huduma bora kwa jamii pia wananchi kutumia kituo hicho kwa kuwafichua wahalifu waliopo kwenye maeneo yao.

Rais Samia akiagana na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Camillus Wambura mara baada ya kufungua Vituo cha Polisi vya Wilaya ya Ikungi pamoja na Mkalama kwenye hafla iliyofanyika Ikungi Mkoani Singida tarehe 15 Oktoba, 2023.
Rais Samia akiwa amesimama wakati wa Heshima ya Wimbo wa Taifa na ule wa Afrika Mashariki mara baada ya kuwasili Ikungi kwa ajili ya ufunguzi wa Kituo cha Polisi cha Wilaya hiyo mkoani Singida tarehe 15 Oktoba, 2023.
Rais Samia akizungumza na Wananchi wa Ikungi waliohudhuria hafla ya ufunguzi wa Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida tarehe 15 Oktoba, 2023.

Leave a Comment