×

Dc Bulembo Awataka Watendaji Wa Mitaa Kufuatilia Na Kusimamia Utekelezaji Wa Miradi Kigamboni

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Halima Bulembo ametoa muda wa mwezi mmoja kukamilishwa kwa ujenzi wa nyumba ya walimu (Two in One) iliyopo katika Shule ya Sekondari ya Pembamnazi inayogharimu Tsh M114 kutoka Serikali Kuu, mara baada ya kubaini uchereweshaji na mapungufu mengi katika ujenzi wa nyumba hiyo ambapo amemuelekeza Kaimu Mkurugenzi kuhakikisha anawasimamia vema Watumishi husika katika usimamizi wa mradi huo.
 
DC Bulembo ametoa maagizo hayo leo tarehe Oktoba 17, 2023 katika ziara yake aliyoianza ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa Wilayani humo ambapo ameongozana na Wajumbe wa Kamati ya Siasa wakiongozwa na Mwenyekiti wa Wazazi Ndugu Greyson Mwinkola aliyemwakilisha Mwenyekiti wa CCM Wilaya hiyo Ndugu Sikunjema Shabani.
 
Katika hatua nyingine, DC Bulembo amekagua mradi wa ujenzi wa kituo cha Afya cha Tundwi Songani wenye thamani ya Tsh Milioni 611 ikiwa Tsh M500 kutoka Serikali Kuu na Tsh M111 kutoka Manispaa ya Kigamboni ambapo ameoneshwa kuridhishwa na hatua zilizofikiwa katika ujenzi huo na kutoa muda wa wiki 3 kwa DMO kuhakikisha majengo hayo ya Jengo la Wagonjwa, Maabara, Wazazi na Upasuaji yanaanza kutoa huduma ipasavyo.
 
Akizungumza mara baada ya kukagua miradi yote zaidi ya 5, DC Bulembo amewataka Watendaji wa Kata na Mitaa kuhakiksha wanapitia na kufuatilia kila hatua katika utekelezaji wa miradi yote kwa kila mtumishi kwenye mtaa wake ilikusudi kuwa sehemu ya kwanza ya kuisaidia Serikali kwenye kubaini mapungufu au changamoto ilikusudi kufanyiwa kuchukuliwa hatua kwa haraka na badala yake waachane na dhana ya kukaa maofisini tu pasipo kujua lolote linaloendelea katika miradi hiyo.

Leave a Comment