
Dar es Salaam, 20 Oktoba 2023: Kupitia ushirikiano wa aina yake, Serengeti Breweries Limited imeungana na Uber kuwapatia ofa kabambe washiriki watakaosafiri kwenda kuhudhuria tamasha la Oktobafest. Ushirikiano huu unalenga kuongeza chachu ya kusherehekea utamaduni wa Tanzania huku ukisaidia kuhamasisha unywaji wa kistaarabu na kuhakikisha usalama wa washiriki wote.
Tamasha la Oktobafest, ambalo limeandaliwa na Serengeti Breweries Limited, litafanyika kwenye viwanja vya Coco Beach tarehe 21 Oktoba 2023. Tamasha hili la kipekee limejizatiti kutoa burudani ya kiutamaduni zaidi, kusherehekea utamaduni wa Tanzania kupitia bia, muziki, mitindo, na chakula.
Habari nzuri ya kuvutia zaidi kupitia ushirikiano huu ni punguzo maalum la 40% kwa safari zote za Uber kwenda na kutoka Oktobafest.
Kupitia Kampeni ya INAWEZEKANA, Kampuni ya Serengeti Breweries Limited inajitolea kuhamasisha unywaji wa kistaarabu, kuhakikisha kwamba washiriki wanafurahia tamasha kwa kistaarabu na hawaweki hatarini usalama wao.
Rispa Hatibu, Meneja wa Mawasiliano na Uendelevu wa Serengeti Breweries Limited, alisema, “Serengeti Lite inajivunia kuandaa Oktobafest, tukio linalosherehekea tamaduni mbalimbali za Tanzania, na tunafurahi kushirikiana na Uber katika jitihada hii. Tunataka washiriki wetu kufurahia tamasha kwa kistaarabu na kwa usalama, na ushirikiano huu unatusaidia kufikia lengo hilo.”
Monica Mziray, Meneja wa Uendeshaji wa Uber nchini Tanzania, amesema, “Kwetu Uber, tunajitahidi kutoa njia za usafiri zilizo rahisi na salama. Ushirikiano wetu na Serengeti Lite kwenye Oktobafest unakwenda sambamba na dhamira yetu. Tunataka wapenzi wa tamasha hili wafurahie wakiwa kwenye tamasha hili huku wakifanya maamuzi ya kistaarabu na kuhakikisha usalama wao kipindi chote cha tamasha.”
Ushirikiano huu wa kimkakati kati ya Uber na Serengeti Lite si tu ni uthibitisho wa dhamira yao kwa jamii, bali pia ni njia ya kuwapatia wasaa wa kipekee wa washiriki wa tamasha hili. Kwa punguzo la kipekee la Uber, washiriki wataweza kusafiri kwenda na kurudi kutoka Coco Beach kwa urahisi, kuepuka hatari za kuendesha wakiwa wamekunywa pombe na kwa usalama wao.
Oktobafest, kama tamasha, linalenga kuunganisha mambo mbalimbali yaliyomo kwenye utamaduni wa Tanzania. Kupitia Kampeni ya INAWEZEKANA ya Serengeti Breweries Limited inahamasisha kutoendesha chombo cha moto ukiwa umekunywa pombe na kutumia safari salama zinazopatikana kupitia Uber, washiriki wanaweza kufurahia tamasha hili la kitamaduni bila wasiwasi wowote.
Kuhusu SBL:
Ilianzishwa mwaka 1988 kama Associated Breweries, SBL ni kampuni ya pili kwa ukubwa nchini Tanzania, na chapa zake za bia zilichukua nafasi ya Zaidi ya 25% ya soko kwa ujazo. SBL ina mitambo mitatu ya uendeshaji iliyopo Dar es Salaam, Mwanza na Moshi.
Tangu kuanzishwa kwa SBL mwaka 2002 biashara hiyo imekuza jalada lake la chapa mwaka hadi mwaka. Upatikanaji wa hisa nyingi na EABL/Diageo mwaka 2010 umeongeza uwekezaji katika viwango vya ubora wa kimataifa na kusababisha nafasi kubwa za ajira kwa watu wa Tanzania.
Chapa za SBL zimepokea tuzo nyingi za kimataifa zikiwemo Serengeti Premium Lager, Serengeti Lite, Pilsner Lager, Guinness Stout, na Guinness Smooth. Kampuni hii pia ni nyumbani kwa vinywaji vikali duniani kama vile Johnniew Walker Whisky, Smirnoff Vodka, Gordon’s Gin, Captain Morgan Rum, Baileys Irish Cream, na chapa zinazozalishwa nchini kama vile Bongo Don SBL’S maiden local spirit brand na Smirnoff Orange.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na:
Rispa Hatibu,
Meneja Mawasiliano na Uendelevu wa SBL,
Simu: +255 685 260901
Barua Pepe: [email protected]
Email: [email protected]