×

Mama’s Beach Party Yafana Dar

Mama’s Day Out  Beach Party wameadhimisha siku ya Afya ya akili  kwa  kuwakutanisha kina mama 170 Jijini Dar es Salaam katika
Kongamano lililoandaliwa na  Kampuni ya Ekima
Insights inayoongizwa  Mkurugenzi wake ambaye ni Mwanahabari mkongwe  Marion Elius .
 Kongamano hilo  linefanyika hivi karibuni katika  ufukwe   Uninio  Jijini Dar es Salaam.
 “Mama’s day  Out Beach Party   imefanyika kwa mara ya pili sasa ambapo tulianza mwaka jana 2022 huku  lengo letu kubwa ni  kutoa elimu
ya kina kuhusu Afya ya Akili katika jamii yetu kwa kupitia wanawake kwa sababu hivi sasa kumekua  changamoto  katika maeneo mbalimbali ya maisha yetu ya  kila siku” amesema Marion.
Mkurugezi  huyo amesema kuwa kongamano hil limefanyika sambamba na
maadhimisho ya Wiki ya Afya ya Akili ambayo huadhimishwa kila ifikapo Oktoba 10 ya kika mwaka huku  kauli mbiu yake ikiwa ni #Jikubali #AnzaUpya. #PendaMaisha” amesema Marion.
Amesema kuwa katika kongamano  hilo kulikuwa na watoa mada mbalimbali  amewataja baadhi yao kuwa ni Mwanasaikolojia maarufu Dkt. Chris Mauki  na wataalamu wabobevu katika masuala ya Afya ya Akili ambao wametoa mada mbalimbali akiwamo
 Bi Caroline Mwanri  , aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi  Communication  na Afisa
Rasilimali  watu  Francis Nanai ambaye amezungumza na kuwapa mbinu wanawake   juu ya suala zima la kujiimarisha kiuchumi na namna ya utunzaji wa fedha    kuwekeza na pia kujiandaa na maisha ya  kustaafu kwani  kumekuwa na wimbi kubwa la wastaafu wengi kupoteza mwelekeo kwa sasa kuwa watanzania wengi hawana elimu ya kujiandaa na kustaafu ambayo imekuwa
ikipelekea watu kupata msongo wa mawazo pindi wanapostaafu.
Mwanasaikolojia
Dkt. Chris Mauki ambaye pia ni  Mhadhiri katika Chuo Kikuu  Cha Dar es Salaam amesema kuwa   wanawake wanauwezo mkubwa wa kuilewa saikologia ya mwanaume na kumudu kuwasaidia afya yao ya akili na kukuza  uwezo vijana wa kiume katika.
Aidha Mwanamtindo na mbunifu wa  mitindo ya mavazi kutoka  Kampuni ya J’adore Ruth Urio amesema kuwa  wanawake wapunguze kuwa na fikra  zinazowapotezea muda wa kufanya  masuala ya maendeleo yao na jamii kwa ujumla.
Katika kongamano  hilo mgeni rasmi alikuwa  Diwani kata ya Kunduchi Mhe. Michael Urioh ambaye amewasisitiza  kina mama hao  umuhimu wa wanawake kuwa  wananafasi kubwa  katika  malezi ya familia na hasa ikizingatiwa tuko kwenye nyakati  ambazo kuna muingiliano wa kimaadili na tamaduni toka
nchi za ng’ambo, hivyo ni muhimu sana kwa wanawake kuwa  jasiri
na thabiti katika malezi hasa ikizingatiwa
kuwa kuna ongezeko kubwa sana la
watoto kulelewa na mzazi mmoja ambao wengi  wao ni wanawake.
Mhe Urioh amesema kuwa  serikali chini ya uongozi wa Rais wetu Mama
yetu Samia  Suluhu Hassan imejikita katika kumuinua mwanamke katika
maeneo mbali mbali na hasa kupatiwa mikopo isiyokuwa na riba na
kuhamasisha wanawake kujitokeza kutumia kikamilifu fursa hizo.
Kongamano  hilo limenogeshwa na michezo mbalibali kama vile kuvuta kamba, kuvumbua  dhahabu huku wakipata zawadi kutoka kwa  Shear Illusion, GSM, J’Adore, Renex, Cassandra
lingerie  The Deck Resturant  .
Aidha muandaaji ametoa shukran kwa Taasisi ambazo waneshiriki kikamilifu ambao ni Hospitali  ya Kairuki Memorial  ya Mikocheni
 Dawasa, Coca-Cola Kwanza, Vodacom, GSM, Renex,
J’Adore na wengine wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine.

Leave a Comment