×

Jokate Awavaa Wabunge Viti Maalum CCM Wasiofanya Mikutano Ya Hadhara, Atoa Tamko – Video

JOKATE Mwegelo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT).

JOKATE Mwegelo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), amewataka wabunge wa viti maalumu kufanya mikutano ya hadhara, ili kusikiliza kero za wananchi.

Amesema, wabunge waliopata nafasi kupitia UWT hawafanyi mikutano ya hadhara kusikiliza kero za wananchi, jambo ambalo linakipa chama chake wakati mgumu wa kujibu tuhuma za wananchi.

Alisema, hayo yamebainika wakati wa ziara ya kamati ya utekelezaji ya UWT.

Alisema, “sisi UWT tumepewa nafasi ya kuchochea uwakilishi wa wanawake kwenye nyadhifa mbalimbali za maamuzi. Ni vyema tukaondokana na ile kasumba kwamba tunajihusisha na wajumbe pekee.”

Kwa mujibu wake, wakati ukifika UWT kitakwenda kumchukulia fomu ya kugombea urais Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kuwa amefanya kazi kubwa ya kuwaingiza wanawake kwenye nafasi za uongozi.

Leave a Comment