Mbunge wa Geita Vijiji, Joseph Kasheku ‘Musukuma’ akichangia mjadala wa uchambuzi wa Ripoti ya CAG amesema kuna fedha nyingi zinatajwa kuibiwa lakini hazionekani kwenye mzunguko wa fedha na kuwa kama zingekuwepo katika mzunguko rasmi zingeweza kutumika katika miradi ya Maendeleo
Amesema “Sehemu nyingi suti zimepanda bei, Tsh. Milioni 1.2, mwingine ananunua hata tano na moka nzuri, ukimkuta ofisini amependeza kumbe mwizi.”
Mbunge Musukuma ameendelea kusema kuwa na wizi wote huu unafanywa na wasomi na kwa maana hiyo anakosa maana kamili ya elimu kwani wasomi wengi ni wezi wa fedha za serikalini.