×

Simbachawene: Kama 5-1 Imetokana Na Rushwa, Simba Mkaripoti Takukuru – Video

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene amesema kama Klabu ya Simba inaamini kupoteza kwa magoli 5-1 dhidi ya Yanga kumechangiwa na mazingira ya Rushwa basi taarifa hiyo ikaripotiwe Ofisi ya TAKUKURU Temeke, Dar es Salaam

Awali, Mbunge Festo Sanga alihoji mpango wa Serikali kukabiliana na Rushwa baada ya kuwa na tetesi za madai ya Rushwa katika mchezo huo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa.

Leave a Comment