
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), imewakamata Watu 16 wanaodaiwa kujihusisha na shughuli za utengenezaji wa Biskuti kwa kuchanganya na Bangi aina ya ‘Skanka’ katika eneo la Kawe
Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas James Lyimo amesema watuhumiwa wamekutwa wakiendelea na uzalishaji wa bidhaa hizo kwa kutumia mtambo mdogo wa kusaga Skanka na vifaa vya kutengenezea Biskuti
Amesema watuhumiwa wamekutwa na Kilo 423.54 za Bangi iliyosindikwa yenye kiwango kikubwa cha Sumu ya ‘TetraHydroCannabinol THC’, ambapo 75% inazalishwa na Bangi aina ya Sativa na 45% Bangi ya Indica ikiwa na sumu zaidi ya 45% ikilinganishwa na 3% hadi 10% zilizo katika Bangi ya kawaida