×

Makonda Atembelea Na Kukagua Daraja La Jpm (Kigogo – Busisi) – Mwanza

Katibu wa Halmashauri Kuu, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Paul Makoda akiongea jambo.

Katibu wa Halmashauri Kuu, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Paul Makonda leo Novemba 12, 2023 ametembelea na kukagua mwendelezo wa Ujenzi wa Daraja la JPM (Kigogo – Busisi) lenye urefu wa Kilomita 3 na Barabara unganishi yenye urefu wa Kilomita 1.66 linalojengwa Wilayani Misungwi.

Kwa mujibu wa Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa amemueleza Mwenezi Makonda kuwa Ujenzi wa Daraja hilo umefikia 80% na mpango wa Serikali ni kuhakikisha hadi kufikia mwezi Agosti mwakani 2024 ujenzi utakuwa umekamilika kwa 100%.

Mwenezi Makonda ameitaka Serikali kuhakikisha inaongeza kasi katika utekelezaji wa Mradi huo.

Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa akimueleza Mwenezi Makonda kuwa Ujenzi wa Daraja hilo umefikia 80%.

Leave a Comment