×

Ishu Ya Adel Kocha wa Viungo Kutua Simba Ipo Hivi

WAKATI tetesi zikieleza kuwa, jina la Adel Zrane aliyewahi kuwa kocha wa viungo wa Simba lipo mezani klabuni hapo, bosi ndani ya timu hiyo amefunguka kuhusu kurejea kwake.

Ikumbukwe kwamba, nafasi ya kocha wa viungo ipo wazi ndani ya Simba baada ya aliyeanza na timu msimu wa 2023/23 Corneille Hategekimana kusiishiwa mkataba wake Novemba 7, mwaka huu.

Mbali na kocha wa viungo, timu hiyo ipo chimbo kumsaka kocha mkuu mpya atakayechukua mikoba ya Roberto Oliveira ambaye alisitishwa mkataba wake ndani ya timu hiyo Novemba 7, 2023.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally, amesema kila kitu kinakwenda sawa, ni suala la muda kutambua nani atakuwa nani katika kikosi hicho.

“Adel amekuwa akitajwa mara nyingi tunapokuwa hatuna kocha wa viungo. Ukweli ni kwamba ni mwalimu mzuri, lakini maamuzi yake yataamuliwa pale uongozi utakapokubaliana nani atakuwa katika nafasi ya kocha wa viungo.

“Atakapotambulishwa mwalimu mpya itakuwa rahisi kuweka kila kitu wazi kwa kuwa kuna mwalimu ambaye anakuja na watu wake na kuna mwalimu ambaye yeye yupo sawa kwa lolote litakalotokea, hivyo tusubiri na tuone,” alisema Ally.

MREMBO APATA GONJWA la AJABU AKIWA CHUO, AKOSA NGUVU, NDOTO za UANASHERIA ZAMLIZA, AOMBA APEWE BIMA

Leave a Comment