×

Taifa Stars Kucheza Dhidi ya Morrocco Uwanja wa Mkapa leo saa 4:00 usiku

KOCHA Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Adel Amrouche, ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa mchezo wa leo dhidi ya Morocco unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Ni saa 4:00 usiku mchezo huo wa Kundi E wa kufuzu Kombe la Dunia 2026, unatarajiwa kuchezwa ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amenunua tiketi zote zilizobaki za jukwaa la mzunguko.

Amrouche amesema: “Tuna mechi ngumu mbele yetu, hilo tunalitambua, kikubwa ambacho tunakihitaji ni kupata ushindi kwenye mchezo wetu. Wachezaji wapo tayari na tunaamini kwamba mchezo wa mpira unahitaji furaha kwa kupata matokeo mazuri.”

Ikumbukwe kwamba, Taifa Stars ilitoka kupata ushindi ugenini kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Marrakech, Morocco, ubao ulisoma Niger 0-1 Tanzania.

Bao pekee la ushindi kwenye mchezo huo wa kufuzu Kombe la Dunia 2026, lilifungwa na Charles M’mombwa akitumia pasi ya nahodha Mbwana Samatta dakika ya 57.

STORI NA LUNYAMADZO MLYUKA

Leave a Comment