×

Aziz Ki, Aucho Washusha Presha Yanga dhidi ya CR Belouizdad

KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Stephane Aziz Ki, Djigui Diarra na Khalid Aucho wamemshusha presha ya Kocha Mkuu wa timu hiyo, Muargentina Miguel Gamondi baada ya kutua kambini juzi usiku tayari kwa mchezo wao dhidi ya CR Belouizdad utakaopigwa leo.

Hiyo ikiwa ni siku moja kabla ya mchezo huo wa hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika utakaopigwa kwenye Uwanja wa 5 July 1962 katika Mji wa Algers.

Mastaa hao wamejiunga na kambi hiyo, wakitokea katika majukumu ya Timu zao za, taifa zilizocheza michezo ya kufuzu Kombe la Dunia.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ali Kamwe alisema kuwa wachezaji woa wote tayari wameripoti kambini tayari kwa ajili ya maandalizi ya mchezo dhidi ya CR Belouizdad.

Kamwe alisema kuwa, baada ya wachezaji hao kuripoti kambini Algiers, walikuwa na siku moja jana jioni Alhamisi ya kufanya mazoezi kwenye uwanja utakaotumika kuchezea mechi.

Aliongeza kuwa kuripoti kwa wakati wachezaji hao, kumepunguza presha ya benchi la ufundi la timu hiyo, linaoongozwa na Kocha Mkuu Muargentina, Miguel Gamondi.

“Kikosi chetu kimekamilika mara baada ya msafara wa tatu kuripoti kambini Algiers, ambao ni Diarra, Aziz Ki na Aucho ambao wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo mgumu na muhimu kwetu kupata ushindi.

“Hautakuwa mchezo mwepesi kwetu na kwao wapinzani wetu, malengo yetu makubwa kuelekea mchezo huu ya kwanza ni ushindi na siyo droo tutakapocheza ugenini ili tufikie malengo yetu makubwa ya kufika katika hatua kubwa.

“Sasa kocha ana maamuzi ya kuamua mchezaji gani amtumie katika mchezo huo, baada ya akina Aziz Ki kuripoti kwa wakati ambao watakuwa na siku moja ya leo (jana) pekee ya kufanya mazoezi,” alisema Kamwe.

STORI NA WILBERT MOLANDI

Leave a Comment