×

Basi la Kampuni ya Allys Star Lagonga treni Mji wa Manyoni mkoani Singida

Habari zilizotufikia asubuhi ya hii leo Novemba 29, 2023 zimeeleza kuwa, watu kadhaa wanahofiwa kufariki dunia na wengine kujeruhiwa katika ajali ya barabarani baada ya basi la Kampuni ya Allys Star kugonga treni katika makutano ya reli na barabara.

Kwa mujibu wa mashuhuda, ajali hiyo imetokea alfajiri ya saa 11:00 nje kidogo ya Mji wa Manyoni mkoani Singida.

Taarifa zilizopatikana eneo la tukio zimeeleza kuwa basi hilo lilikuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Mwanza na kwamba Polisi walifika mara moja eneo la tukio kwa ajili ya uokoaji na jeshi hilo litatoa taarifa kamili baadaye.

Kwa updates zaidi za tukio hilo endelea kuwa karibu na GLOBAL TV.

Leave a Comment