×

Serikali Kwa Ushirikiano na Wadau wa Hamburg Kuimarisha Bustani za Majiji

SERIKALI kwa kushirikiana na wadau kutoka nchi ya Hamburg ,wameonyesha dhamira ya uboreshaji wa bustani mbalimbali zilizopo katika miji  ikiwemo mji wa Dar es Salaam ambao itawasaidia kuongeza pato ya nchi kwa kupitia watalii wanaoingia nchini.
Akizungumza Jana  wakati wa uzinduzi wa warsha ya uboreshaji wa Bustani ya Botanical iliyopo Dar es Salaam Ofisa Mtendaji wa Kata hiyo Majura Mtalemwa, amesema wataalam kutoka jiji la Hammbarg nchini Ujerumani wamefika nchini kwa lengo la kusaidia  utoaji wa elimu na jinsi ya kuendesha bustani.
Mtalemwa alisema uboreshwaji wa Bustani hizo ni chachu kubwa ya kuja kuongeza mapato kwa taifa kwani watu watakuwa wanafika katika maeneo hayo na kupumzika au kuangalia viungo mbalimbali ambavyo vimepandwa katika  Bustani hizo.
Alisema miaka mingi bustani hizo zilikuwa zinaendeshwa bila ya kuingiza faida yeyote,hivyo ushirikiano huo utasaidia na kuongeza chachu kwa Jamii kufika katika maeneo hayo kupumzika au kujisomea kwa wanafunzi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mali kale ya Makumbusho Rivocatus Ligumba alisema eneo la bustani Botanical ni eneo la kihistoria toka enzi za zamani.
Alisema maeneo ya bistani muhimu duniani kote kwa sababu zina historia nyingi ambazo ni faida kwa vizazi vijavyo.
“Eneo kama hili wanafunzi wanakufa nakufanya masomo yao kwa vitendo kwa kujua mti fulani unafaida gani? Na nini chimbuko lake,”alisema
Naye, Seneta kutoka mji wa Hamburgn anaeshughulikia masuala yanayohusu nchi ya Afrika,Dkt Anna Catarina Seboda  alisema wanamahusiano mazuri na Tanzania tangu miaka 12 iliyopitia katika masuala mbalimbali ikiwemo kupeana uzoefu wa jinsi ya kutunza bustani na miji.
Alisema hivi sasa wamekuja na wataalam wao ambao kazi kubwa itakuwa ni kuboresha bustani ya botanical kwa lengo la kuongeza pato nchini na kuongeza kasi ya Watalii nchini.
Alisema si kuongeza pato peke yake ila bustani hiyo ikifanyiwa ukarabati watu wengi zaidi watafika kwa lengo la kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo miti iliyopo ndani ya bustani hiyo.

Leave a Comment