Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema linawashikilia askari wake wawili kwa tuhuma za kumpiga risasi Razack Azzan, mlinzi wa baa ya Board Room iliyopo Sinza Mapambano jijini Dar es Salaam.
Jeshi hilo limeeleza kwamba lilipokea taarifa za kutokea kwa tukio hilo Novemba 29, 2023 majira ya saa sita usiku ambapo askari walimjeruhi mlinzi huyo ambaye baadaye alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu.
“Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa Mwananyamala kukamilisha uchunguzi,” imeeleza taarifa hiyo.