
Shirikisho la Soka Afrika (CAF) usiku wa kuamkia leo Decemba 1, 2023 limezindua Chama cha vilabu vya soka Barani Afrika (ACA) likimchagua Mtanzania na Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Hersi Said kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chama hicho chenye makao yake makuu Nairobi Kenya.
Injinia Hersi atasaidiwa na Jessica Motaung wa Kaizer Chiefs kama makamu Mwenyekiti huku Paul Basset wa Akwa United ya Nigeria akichaguliwa kuwa makamu Mwenyekiti wa pili.
Uzinduzi huo uliofanyika Nchini Misri umesimamiwa na Rais wa CAF, Patrice Motsepe nchini Misri huku Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Simba SC, Salim Try Again akiwa miongoni mwa waliohudhuria.