×

Majaliwa Awatembelea Majeruhi wa Maafa ya Maporomoko ya Tope Hanang

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Desemba 05, 2023 amefika kuwajulia hali majeruhi wa maafa ya mafuriko yaliyosababisha kuporomoka kwa tope na mawe kutoka Mlima Hanang, Katesh Mkoani Manyara.

Majeruhi hao wanapatiwa matibabu bure na Serikali katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara, ikiwa ni maelekezo yaliyotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Leave a Comment