×

Medeama, Yanga Hakuna Mbabe, Mechi Yaisha Kwa Sare Ya 1-1

MAGOLI yaliyofungwa na Jonathan Sowah wa Medeama na Pacome Zouzoua wa Yanga yameziwezesha timu hizo kutoka sare ya goli 1-1 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Kundi D uliopigwa kwenye Uwanja wa Kumasi Nchini Ghana

Mchezo mwingine wa Kundi hilo AlAhly ya Misri imepata matokeo ya 0-0 dhidi ya CBelouizdad yaAlgeria

Baada ya mechi hizo, Al Ahly inaongoza ikiwa na pointi 5, CR Belouizdad (4), Medeama (4) na Yanga ina (2)

Michezo inayofuata Belouizdad itaikaribisha Al Ahly (Desemba 19, 2023), Yanga itakuwa mwenyeji wa Medeama (Desemba 20, 2023)

FT: MEDEAMA 🇬🇭 1-1 🇹🇿 YANGA SC
⚽ Sowah ( P) 26’
⚽ Zouzoua 36’

FT: Al Ahly 🇪🇬 0-0 🇩🇿 CR Belouizdad

MSIMAMO KUNDI D
1. 🇪🇬 Al Ahly (pointi 5)
2. 🇬🇭 Medeama (4)
3. 🇩🇿 CR Belouizdad (4)
4. 🇹🇿 Yanga SC (2)

Kuna tofauti ya alama tatu kati ya kinara Al Ahly ya Misri na washika mkia Young Africans SC, bado nafasi ipo.

Leave a Comment