
Mchezo mpya wa CHEZAUSHINDE, unaoendeshwa na Airtel Money kwa kushirikiana na Whiteball leo wamemkabidhi rasmi mshindi wa kwanza wa Jackpot ya wiki katika msimu huu wa sikukuu Bw. PAMELA KAHISE aliyejishindia pikipiki mpya.
Mchezo wa CHEZAUSHINDE ambao ni maalumu kwa wateja wa Airtel pekee, unatoa fursa kwa wateja kujishindia pesa taslimu, simu, TV na pikipiki kupitia droo za kila saa, wiki na kila wiki.
Mshindi huyo amefanikiwa kushinda kwa kucheza moja ya michezo ya CHEZAUSHINDE (Pesachap, Piga Mkwanja,Jackpot na Shinda Mnada).

Namna ya kushiriki mchezo wa CHEZAUSHINDE:
- Bonyeza menu ya AirtelMoney: *150*60#
- Chagua namba 5: Lipia Bili
- Chagua namba 6: Bahati Nasibu
- Kisha Chagua namba 2: Gaming
- Kisha Chagua namba 1: CHEZAUSHINDE
- Baada ya hapo unaweza kuchagua mchezo wowote kati ya michezo 5 iliyopo uweze kujishindia
- Kushiriki ni shilingi 1,000 tu.
Akizungumzia ushindi wake wa pikipiki, Bw. PAMELA KAHISE amesema anaishukuru Airtel Money kwa kumpa nafasi ya ushindi.
‘Sikutarajia kabisa kushinda pikipiki kwani hii itanisaidia kwenye shughuli zangu na biashara. Nawashukru sana Airtel Money na CHEZAUSHINDE kwa uaminifu wenu na kwa fursa kama hizi mnazozitoa kwa watanzania na nawashauri watanzania wenzangu washiriki CHEZAUSHINDE ili nao wanufaike na ushindi huu’ alisema bwana Kahise.
Kwa upande wake, Meneja Mahusiano wa Airtel, bwana Jackson Mmbando amesema kwenye msimu huu wa sikukuu CHEZAUSHINDE itatoa zawadi za pesa, simu na TV kwa watanzania wengi zaidi.
‘Msimu huu wa sikukuu kila mmoja ni mshindi. Unachaotakiwa kufanya ni kucheza gemu yoyote kwenye CHEZAUSHINDE ili uingie kwenye droo za kushinda zawadi hizi kama bwana Kahise’ alisema bwana Mmbando.
Kwa maelezo zaidi:
Tembelea kurasa zetu katika mitandao ya kijamii: Instagram na Facebook (CHEZAUSHINDE)
#CHEZAUSHINDE #USHINDINJENJE