×

Kimzaamzaa, Jamaa Waula Mamilioni Ya Fedha Magifti Dabodabo Droo Ya Nne

Semaji la Kampeni ya Magifti Dabo dabo, Haji Manara wapili kulia akiwa na washindi wa droo ya nne waliokabodhiwa mamilioni yao leo.

Dar es Salaam, 15 Desemba 2023: Unachoweza kusema kiurahisi ni kwamba Jamaa wameula kimzaamzaa mamilioni ya Kampeni ya Magifti Badodabo. Luhuvilo Magombola mkazi wa Mabibo, David Bombeki mwanachuo DIT, na Janeth Emmanuel Mghweno mkazi wa Shekilango Dar Es Salaam, wameingia kwenye Orodha ya washindi wa mamilioni ya fedha kutoka kampeni ya MAGIFTI DABO DABO inayoendelea hivi sasa, Luhuvilo na David wameshinda milioni moja moja na Janeth ameshinda Milioni Tano ambapo washindi hawa wanaingia kwenye Orodha ya Washindi 50 Hadi hivi sasa wa Kampeni hii.

Ikumbukwe Kampeni hii inayoendeshwa na Kampuni ya Tigo imezinduliwa wiki kadhaa zilizopita huku ikimtambulisha Haji Manara kama SEMAJI la Kampeni hii, ambapo mteja wa Tigo anaweza kushinda Fedha Taslimu hadi Milioni 10, Safari ya Kwenda Dubai au Zanzibar, Set ya Vifaa vya Ndani ambavyo ni Sound bar, Friji, TV na Microwave na Zawadi kubwa ya Magari Mawili ( 0km ) , kingine kinachovutia katika kampeni hii ni kwamba ukishinda kitu kimoja wapo kati ya ivyo unamchagua na yeyote umpendae ili apewe zawadi iyoiyo uliyoshinda hii ndio maana halisi ya MAGIFTI DABO DABO.

Meneja wa Wateja Maalum Tigo Pesa, Mary Rutta (kushoto) akimpongeza Janeth Emmanuel Mghweno wakati akimkabidhi mfano wa hundi ya milioni tano aliyojishindia.

Akizungumza baada ya kuwakabidhi mfano wa Hundi washindi hawa  Meneja wa Wateja Maalum Tigo Pesa Bi Mary Rutta  amewasisitiza Watanzania kufanya miamala mbalimbali na Tigo Pesa ili kuibuka washindi maana kampeni bado inaendelea.

“Muda huu tunaozungumza kuna washindi 15  wanarudi leo hii kutoka DUBAI, na  wengine wamerudi jana kutoka Zanzibar lakini bila kusahau kuna wengine wamejishindia Pesa Taslimu na wapo pia wamejishindia Vifaa vya Hisense kwahyo kampeni bado inaendelea fanyeni miamala na TIGO PESA kwa wingi, Lipa kwa Simu, nunua vifurushi ili utengeneze mazingira ya kuibuka Mshindi ” alisema Mary Rutta.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti washindi wameipongeza tigo kwa kuwakumbuka wateja wake kupitia kampeni mbalimbali, Aidha wamewasihi watanzania kufanya miamala na Tigo Pesa maana ndo Siri pekeee ya Ushindi.

Leave a Comment