
Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao ikiongozwa na mwenyekiti wake, Steve Mengele @stevenyerere2 leo Desemba 15, 2023 imeanza rasmi ziara yake mkoani Manyara kuwatembelea waathirika wa maporomoko ya tope yaliyotokea wilayani Hanang, Manyara.

Taasisi hiyo imewatembelea na kuwapa mkono wa pole waathirika hao katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara ambapo baadhi wanaendelea kupatiwa matibabu katika wodi ya wanaume, wodi ya wanawake na wodi ya watoto.
Waathirika hao wameishukuru taasisi hiyo ambayo ni ya kwanza ya wasanii kuwatembelea na kuwapa mkono wa pole.

Sambamba na hilo, wameendelea kutoa shukrani zao kwa Rais Samia Suluhu Hassan na serikali yake kwa kuendelea kuwahudumia kuanzia mwanzo mpaka hivi sasa.