×

Mbunge Janeth Masaburi Awaahidi Masoko Ya Kisasa Wana Temeke, Awapa Bure Mama Lishe Majiko Ya Gesi

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dar es Salaam, Janeth Masaburi (mwenye miwani) akitembelea masoko.

Dar es Salaam 21 Desemba 2023: Serikali  ya Halmashauri ya Manispaaya Temeke imesema inampango wa kuboresha masoko yake makuu ikiwemo solo la Temeke Sterio, Tandika na Keko yaweze kufanana kama solo kuu la Kariakoo.

Akizungumza na wafanyabiashara wa Soko la Temeke Sterio, Tandika na Keko kwenye ziara yake iliyofanyika jana kwenye Wilaya ya Temeke, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dar es Salaam, Janeth Masaburi alisema masoko hayo yakikarabatiwa yataweza kuwa kivutio na ongezeko la wateja kutoka ndani na nje ya nchi kuja kununia bidhaa kwenye soko hilo.

Akigawa majiko ya gesi kwa mama lishe.

“Haya masoko natumaini yatakuwa ni masoko ya mfano kwa sababu yatakwenda kuleta wateja wengi Sana, kwa hiyo nawaomba viongoozi wa masoko mlisimamie hili”alisema Mheshimiwa Janeth.

Pia mbunge Janeth aliwakumbusha wafanabiashara wa masoko hayo kuzingatia suala la usafi katika maeneo yao wanayofanyia biashara ili kisudi maeneo yao yao yawe kivutio kwa watu wanaofika kutembelea masoko hayo kwa kununua bidhaa pamoja na wafanabiashara wenyewe kuepukana na magonjwa ya mlipuko.

Mbunge Janeth Masaburi pia alitoa majiko ya gesi na mkaa mbadala kwa mama lishe na baba lishe wanaofanya biashara ya kuuza chakula kwenye masoko hayo ili kisudi waweze kuachana na matumizi ya kupikia kuni na mkaa unaosababishwa na kuni.

Mbunge Janeth Masaburi akiangalia matunda kwenye moja ya masoko aliyotembelea.

Naye Meneja wa Masoko ambaye pia ni Msimamizi Mkuu wa masoko yaliyopo kwenye wilaya ya Temeke Godfrey Asukile alisema ukarabati wa masoko hayo matatu Temeke Sterio, Tandika na Keko unatarajia kufanyika mwanzoni mwakani na unatarajia kugharimu zaidi ya shilingi Milioni 600.

Mbunge Masaburi na msafara wake wakielekezana jambo na mama lishe.

Aidha alisema masoko hapo pia yanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa mapaa machajavu ya soko, mitaro , kizimba cha taka na uongezaji wa matundu ya vyoo pamoja na miundombinu ya soko kwa ujumla.

Mbunge Janeth anafanya meendelezo ya ziara yake ambapo Disemba 6 mwaka huu, kwa kufanya ziara kwenye kata ya Pugu, Jimbo la Kibamba na  Ubungo, Jimbo la Kawe  wilaya ya Kinondoni na Jimbo la Temeke wilaya ya Temeke Mkoa wa Dar es Salaam.

Leave a Comment