×

Washindi 9 wa maokoto Ndani ya Kizibo Waondoka na Laki Tano Kila Mmoja

Washindi 9 wa raundi ya 10 ya kampeni ya Maokoto Ndani ya Kizibo inayoendeshwa na Kampuni ya Serengeti Breweries (SBL) wametangazwa ambapo kila mmoja ameibuka na fedha taslimu, shilingi 500,000 (laki tano).

Washindi waliotangazwa ni Khadija Hamisi wa Kigamboni, Dar es Salaam, Devotha Mwalaumbo wa Bagamoyo, Pwani, Samuel Agustino wa Sinza jijini Dar es Salaam na Paul Mrema wa Vunjo, Moshi mkoani Kilimanjaro.

Wengine ni Catherine John wa Kyela, Mbeya, Moses Makula wa Mwanza, Mohamed Paul wa Tabora, Chrizantus Ngwesa wa Mzumbe, Morogoro na Joyce Godfrey wa Vunjo, Moshi ambao wamekabidhiwa zawadi zao na wawakilishi wa mikoa husika.

Leave a Comment