×

Waziri wa Maliasili na Utalii Angellah Kairuki na Katibu Wake Dkt Abbasi Wafika Handeni

Katika kukamilisha Mwaka Disemba 31, 2023, Waziri wa Maliasili na Utalii Angellah Kairuki pamoja na Katibu Mkuu, Dkt. Hassan Abbasi na watendaji wengine akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Albert Msando, wamefika Msomera, Handeni ambako uwekezaji na uwezeshaji wa kihistoria unaendelea chini ya Serikali ya Awamu ya Sita mahali wanapohamia wakazi wa Ngorongoro kujiridhisha kuhusu ujenzi wa nyumba 5,000 na miundombinu mingine tayari kuendelea kuhamisha wakazi walioko ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro kuja hapa.

Katika kuwahamisha wakazi hao Serikali inafanya haya

1. Kila kaya inapewa nyumba ya vyumba vitatu;
2. Fidia ya maendelezo wanakotoka;
3. Fedha ya usumbufu;
4. Eneo la eka 2.5 la kiwanja chenye hati;
5. Shamba eka 5 na hati;
6. Gharama za usafiri wa familia nzima na mifugo kutoka Ngorongoro hadi hapa
7. Chakula cha miezi 18 ya mwanzo tangu kuhamia.

Na bado, Serikali inajenga na kuhakikisha huduma hizi eneo jipya ambazo kule Ngorongoro ama kisheria; kwa sababu za sheria za ndani au kimataifa za uhifadhi ilikuwa hawapati au haziruhusiwi kuwekwa sasa Msomera watapata pia:

1. Barabara nzuri za mitaa kwa sasa zaidi ya km 150 tayari na zitafika km 800
2. Maji zaidi ya visima 10 vishachimbwa
3. Umeme unaendelea kusambazwa
4. Shule ya msingi ishajengwa na nyingine moja ya Sekondari na moja msingi zinakuja
5. Shule moja ya sekondari na maabara ya kisasa ya kompyuta inakamilika
6. Huduma za afya zahanati tayari na inaboreshwa nyingine
7. Vituo vya polisi kimoja tayari cha daraja B kinakuja
8. Mnada wa mifugo ushajengwa unakamilika
9. Mashamba ya malisho yashapimwa na shamba darasa limeanza
10. Mabwawa na maeneo ya kunywesha mifugo mawili yanajengwa moja limeshajaa maji bwerere na vituo vya kunyweshea vishaanza kazi
11. Vituo vya kuuzia maziwa vinajengwa
12. Huduma za ustawi wa jamii
14 Kunajengwa kituo maalum kuhudumia watoto waliofanyiwa ukatili
15. Kunajengwa kituo cha huduma za pamoja (One Stop Center)
16. Maghala ya kuhifadhia malisho na raslimali za mifugo
17. Minara ya mawasiliano imewekwa
18. Kanda maalum zimetengwa ikiwemo korido za wanyamapori, malisho, biashara mbalimbali, michezo n.k.
19. Viwanja 5,648 vimeshapimwa Msomera (Handeni), Saunyi (Kilindi) na Kitwai (Simanjiro); na

20. Wanawekewa mpaka “wiring” ya umeme nk.

Leave a Comment