
Aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Burundi “BRB” Dieudonné Murengerantwari, ameachiwa huru ikiwa ni miezi mitatu baada ya kupelekwa katika Gereza Kuu la Mpimba mjini Bujumbura.
Dieudonné Murengerantwari alikamatwa tarehe 7/10/2023 kwa shutuma za uhujumu uchumi,rushwa na matumizi mabaya ya madaraka.
Kabla ya kuhamishiwa katika gereza kuu la Mpimba alikuwa amepelekwa katika gereza la kijasusi kwa ajili ya uchunguzi zaidi.