×

Majaliwa: Shilingi Bil. 48 Zimetengwa kwa ajili ya kutoa mikopo Wanafunzi Wa Stashahada

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akifungua kitambaa kuashiria uzinduzi wa Chuo Kikuu Katoliki Mbeya, wakati wa hafla iliyofanyika chuoni hapo Januari 16, 2024 Mkoani Mbeya. Kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Askofu Gervas Nyaisonga na wapili kushoto ni Cardinal Mstaafu Askofu Polycap Pengo

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema katika mwaka wa masomo 2023/2024 Serikali imetenga Sh. bilioni 48 kwa ajili ya kutoa mikopo kwa wanafunzi wa ngazi ya stashahada.

Amesema hayo Jumanne, Januari 16, 2024 wakati wa ufunguzi wa Chuo Kikuu Katoliki Mbeya (CUoM) mkoani Mbeya.

Amesema kuwa mpango huo ambao ni maono na maelekezo ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan unalenga kuhakikisha elimu inayotolewa inakuwa bora na kuwezesha wahitimu wa vyuo nchini kujiamini na kumudu ushindani wa kitaifa na kimataifa.

“Lengo jingine la Mheshimiwa Rais Dkt. Samia ni kuona vijana wengi wanapata elimu itakayowapa ujuzi na uwezo wa kushiriki katika ujenzi wa Taifa”.

#EXCLUSIVE: KARATA COMEDIAN ANAYETRENDI MITANDAONI – AFICHUA MAZITO YALIYOMPATA AKITAFUTA U-STAR…

Leave a Comment