×

Mkurugenzi wa Bandari Afunguka “Hakuna Sukari iliyokwama Bandarini” – Video

Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Mrisho S. Mrisho.

MKURUGENZI wa Bandari ya Dar es Salaam, Mrisho S. Mrisho ameweka wazi kuwa kama sehemu ya matokeo ya uchapakazi, nidhamu na usimamizi mzuri wa menejimenti wamefanikiwa kuandika rekodi mpya ya kuhudumia zaidi ya Tani Milioni 2.5 kwa mwezi.

Mrisho amesema ongezeko hilo limeshuhudiwa kuanzia mwezi Oktoba mwaka jana ambapo zaidi ya makontena 90,000 yanahudumiwa kwa mwezi, tofauti na awali ambapo walikuwa wakihudumia mzigo wa Tani Milioni 1.6 pekee.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Jumapili jijini Dar es Salaam, Mrisho amesema: “Napenda kuwahakikishia Watanzania kuwa shughuli za bandari zinaendelea vizuri ambapo katika kipindi cha siku nne pekee za mwezi huu Februari tayari tumehudumia meli zaidi ya 10.

“Lakini pia ningependa kukanusha baadhi ya taarifa kuhusu suala la mizigo kukwama hapa bandarini, ukweli ni kuwa kwa sasa tumeandika rekodi mpya ya kuhudumia makontena zaidi ya 90,000 kwa mwezi yenye mzigo wa zaidi ya Tani Milioni 2.5 kulinganisha na Tani Milioni 1.6 za awali.

“Ikumbukwe hivi karibuni pia kwa kushirikiana na Bodi ya Sukari tulifanya upakuaji wa dharula wa shehena kubwa ya sukari.”

Leave a Comment