×

Mwanamfalme Harry Kuelekea London Kumuona Baba Yake

Mwanamfalme Harry wa Uingereza akiwa na mke wake Meghan.

OFISI ya Mwanamfalme Harry wa Uingereza imethibitisha kuwa atasafiri kwa ndege hadi London kumuona baba yake .

Mfalme aliiambia familia yake kibinafsi juu ya utambuzi wake wa saratani, Ikulu inasema.

Hatujui ni lini Harry atawasili Uingereza, lakini anatarajiwa kuondoka California hivi karibuni.

Mwanamfalme anatarajiwa kuwasili London peke yake.

Mkewe Meghan atasalia Marekani na watoto wawili wa wanandoa hao – mwanamfalme Archie na Bintimfalme Lilibet.

Ziara ya Harry imeibua matumaini ya maridhiano ndani ya Familia ya Kifalme.

KAMWE APATA KIGUGUMIZI SWALI la GOLIKIPA MSHERY, STRAIKA MPYA GUEDE MABADILIKO YANGA..

Leave a Comment