×

Rais Samia Alivyowasili Ethiopia kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Feburuari 17, 2024 amewasili Addis Ababa Nchini Ethiopia kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika, safari ambayo ameifanya baada ya kutoka kijijini Ngarash Wilayani Monduli Mkoani Arusha ambako ameongoza Waombolezaji kwenye maziko ya Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Edward Lowassa.

Rais Samia amesema katika mkutano huo wa Ethiopia, pamoja na mambo mengine watajadili kuhusu amani na usalama wa Nchi za Afrika, na sera na majawabu kuhusu elimu na ujuzi, ikiwa ni maeneo yanayogusa maisha ya Wakazi zaidi ya bilioni moja wa Nchi Wanachama.

Leave a Comment