×

Rais Samia Awapongeza Ramadhani Brothers kwa Kuibuka washindi katika shindano la America’s Got Talent

Rais Samia Suluhu Hassan

Rais Samia Suluhu Hassan leo Februari 20, 2024 amewapongeza The Ramadhani Brothers kwa kuibuka washindi katika shindano la America’s Got Talent: Fantasy League.

Kupitia ukurasa wa Twitter na Instagram, Rais ameandika “Pongezi kwa vijana wetu Fadhili na Ibrahim (The Ramadhani Brothers) kwa kuibuka washindi katika mashindano ya sanaa na burudani ya AGT: Fantasy League. Safari yenu inaendelea kudhihirisha kuwa juhudi, nidhamu, kujituma na kujiamini ni nguzo muhimu kufikia mafanikio. Mnaitangaza vyema nchi yetu na kuweka mfano bora kwa wengine.”

Leave a Comment